Mtume wa Mwenyezi Mungu (Rehma na Amani ziwe juu yake na Aali zake) amesema: "Mwenye kuisoma Ayat al-Kursi akiwa amelala, basi Mwenyezi Mungu atamlinda yeye na nyumba yake na nyumba za jirani zake”(1).
Imamu Sadiq (a.s) anasema: Kila kitu kina kiini (kilele au sehemu ya juu na iliyokuwa bora zaidi), na kiini na kilele cha Qur'an Tukufu ni Ayat al-Kursi. Yeyote atakayeisoma kwa mara moja tu, Mwenyezi Mungu atamuondoshea taabu (masaibu) elfu moja katika masaibu (mabalaa) ya Dunia, na (taabu au) masaibu elfu moja katika masaibu ya Akhera. Masaibu (balaa) nyepesi kabisa katika masaibu ya duniani ni – Umasikini – “Ufukara”, na masaibu mepesi (ya daraja ya chini) kabisa ya Akhera ni “Adhabu ya kaburi”, nami ninaisoma Ayatul – Kursi kwa matumaini (na kwa malengo) ya kuboresha – na kuinua – daraja na hadhi yangu”(2).
Kwa mujibu wa maneno ya Mtukufu Mtume Muhammad (Rehema na Amani ziwe juu yake na Aali zake), mteule wa Qur’an (yaani: Surah iliyoteuliwa zaidi na kupewa ubora wa juu zaidi) ni Surat al-Baqarah, na mteule wa Suratul-Baqarah ni Ayat al-Kursi (3), na Aya hiyo ni moja ya Aya za Qur’an Tukufu ambazo ni mashuhuri zaidi, ambazo zimezingatiwa katika nyanja mbalimbali.
Mtume wa Uislamu (Rehema na Amani ziwe juu yake na Aali zake) amesema: “Mwenye kusoma Ayat al-Kursi baada ya Swala ya Faradhi, huyo yuko chini ya (himaya) ulinzi wa Mwenyezi Mungu mpaka wakati wa Swala nyingine” (40).
Imam Baqir (a.s) anasema: “Yeyote anayesoma Ayat al-Kursi baada ya kutawadha (baada ya kutia udhu), Mwenyezi Mungu atampa malipo ya [ibada za] miaka 40, atampandisha (atamnyanyua) digrii (daraja) 40, na atampa Hurul Ayni 40” (5).
Imam Ali (a.s) anasema: “Wakati wowote Muumini anapoisoma Ayat al-Kursi na kuwagawia wafu (waliotangulia mbele ya haki) thawabu zake, Mwenyezi Mungu humuwekea Malaika kwa kila herufi moja ya Ayat al-Kursi ambao hufanya amali ya kumtukuza (na kumsabihi) Mwenyezi Mungu kwa ajili yake mpaka Siku ya (Kiyama) Hukumu (6).
Imam Baqir (a.s) anasema: “Yeyote anayesoma Ayat al-Kursi akiwa amesujudu, hataingia kwenye moto wa Jahannam” (7).
Imam Sadiq (a.s) anasema: “Unapokuwa mahali pa kutisha; Soma Aya hii:
﴿وَقُل رَّبِّ أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَل لِّي مِن لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا﴾ “BWANA akasema, Nitaleta haki, nami nitaleta haki, na kunifanya mtawala wa adui zako” (8):
“Na sema: Ewe Mola wangu Mlezi! Niingize [katika kila jambo] kwa uaminifu (na kiukweli), na unitoe nje [ya kila jambo lisilostahili] nitoke (kiukweli), na unipe kutoka kwako msaidizi (hoja) ya kuninusuru (au kunisaidia)”.
Maana nyingine ya Aya hiyo iliyokuwa wazi zaidi:
“Na sema: Mola wangu Mlezi! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazo toka kwako zinisaidie”(80).
Na unapoona jambo la kutisha (linakuelekea au linakukabili), basi soma Aya ya Ayatul-Kursi (9).
Imam Sadiq (a.s) alisema: “Anza safari yako kwa kutoa Sadaka au kwa kusoma Ayat al-Kursi” (10).
Imekuja ndani ya Kitabu cha al-A’mali cha Sheikh Sadouq (amani iwe juu yake) kwamba Amirul-Mu’minina Ali (a.s) alisema: “Lau ugelijua ni jinsi gani Ayat al-Kursi ilivyokuwa na umuhimu na tahamani kubwa, basi kwa hakika hutoiacha Ayatul – Kursi kwa hali yoyote ile”.
Jikinge kwa Ayatul - Kursi ili kutatua na kuondoa matatizo yako, ikiwa una shida au ikiwa umenasa (umekwama kwenye jambo lolote), ikiwa wewe ni mgonjwa, na ikiwa milango yote ya dunia imefungwa mbele yako, basi ni kwa nini (unaghafilika) kuisoma Ayatul - Kursi?!. Soma Ayatul – Kursi kwa imani na itikadi kamili na hatimaye uyafikie matokeo yake (au ufikie hitimisho la matatizo yako) , kama vile (wengine) walivyoisoma Ayatul - Kursi na wakafikia hitimisho (la matatizo yao).
_
Tanbihi na Vyanzo:
1- Mustardak al-Wasail, juzuu ya 1, uk 343.
2- Aya’shi, Muhammad bin Masoud, Kitab al-Tafseer, juzuu ya 1, uk 136.
3- Tabrasi, Fadhli bin Hassan, Majma al-Bayan fi Tafsir al-Qur'an, pamoja na utangulizi wa: Balaghi, Mohammad Jawad, juz 2, uk 626.
4- Lakhmi Tabarani, Suleiman bin Ahmed, Al-Mu'jam al-Kabir, juzuu ya 3, uk 84.
5- Shayiri, Muhammad bin Muhammad, Jame Al-Akhbar, uk 45.
6- Deilmi, Hasan bin Muhammad, Irshad al-Qulub hadi al-Sawab, juzuu ya 1, uk 176.
7- Jame Al-Akhbar, uk 46.
8- Suratul - Isra, Aya ya 80.
9- Barqi, Ahmed bin Muhammad, Al-Mahasen, Mohaghegh, Muhadath, Jalaluddin, juzuu ya 2, uk 36.
10- Furuu al-Kafi, juzuu ya 4, uk 283.